Upfield ni kiongozi wa kimataifa katika lishe inayohusiana na mimea na historia na wasifu wa chapa, ikiwemo Flora, Rama, Becel, Blue Band, Country Crock, I Can’t Believe it’s not Butter na ProActiv.
Tunajua kuwa unajali kuhusu data yako ya binafsi na jinsi inavyotumiwa na tunataka uamini kuwa Upfield hutumia data yako ya binafsi kwa uangalifu. Ilani hii ya Faragha itakusaidia kuelewa data ya binafsi tunayokusanya, sababu tunayoikusanya na jinsi tunavyoitumia.
Unaposoma Ilani yetu ya Faragha, tafadhali fahamu kuwa inatumika kwa Upfield B.V. na kampuni zote za Upfield Group ("Upfield").
Upfield Europe B.V. ni mdhibiti wa data wa data ya binafsi tunayokusanya kwenye tovuti ya www.upfield.com. Upfield Europe B.V. au asasi ya karibu ya Upfield itakuwa mdhibiti wa data wa data ya binafsi tunayokusanya kwenye tovuti mahususi ya chapa ya karibu (kwa mfano, https://www.flora.com/ au https://www.fruitdor.fr/).
Tafadhali chukua muda ujifahamishe desturi zetu za faragha na utufahamishe ikiwa una maswali yoyote kwa kututumia barua pepe au kuwasilisha ombi kupitia fomu ya “Wasiliana Nasi” kwenye tovuti yetu.
Ikiwa unataka kujua ni Maelezo Yapi ya Kibinifasi / Data ambayo Upfield inayo kukuhusu, tafadhali wasilisha ombi hapa.
Ikiwa unataka Upfield iondoe Maelezo Yote ya Kibinafsi / Data ambayo inawezekana kuwa wako nayo kukuhusu, tafadhali wasilisha ombi hapa.
Ilani hii ya Faragha inatumika kwa data ya binafsi iliyokusanywa na Upfield kuhusiana na bidhaa tulizo nazo na matumizi ya tovuti hii.
Data ya binafsi inamaanisha taarifa yoyote inayohusiana na mtu aliyetambuliwa au anaweza kutambuliwa. Ufafanuzi huu unajumuisha data ya binafsi iliyokusanywa nje ya mtandao au mtandaoni kupitia vituo vyetu vya ushirikishaji wa wateja, kampeni za kutafuta soko za moja kwa moja, mashindano, tovuti, programu na kurasa za chapa kwenye mifumo mingine, programu zinazofikiwa au kutumiwa kupitia mifumo mingine na mifumo yetu ya kuajiri / maombi ya kazi.
Tunaweza kukusanya data ya binafsi kutoka vyanzo mbalimbali. Hii inajumuisha:
Data ya binafsi unayotupa moja kwa moja.
Tunakusanya data ya binafsi unayotupa unapojisajili ili kupokea jarida la kutafuta soko, kukamilisha utafiti, kuingia kwenye shindano, kuwasiliana nasi kupitia tovuti zetu au mifumo mingine ya mtandaoni. Kwa kufanya hivyo, unaweza kutupa data ya binafsi, kwa mfano:
Baadhi ya chapa za Upfield zinaweza kukusanya “kategoria maalum za data ya binafsi” kukuhusu (kwa idhini yako dhahiri). Kwa maelezo zaidi kuhusu kategoria maalum za data tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia, tafadhali rejelea sehemu muhimu hapa chini.
Kama sehemu ya shughuli za kuajiri wafanyakazi wetu, tunakusanya data ya binafsi unayotupa wakati wa kutuma ombi la wajibu kwenye Upfield. Kwa mfano:
Data ya binafsi tunayokusanya kiotomatiki.
Pia tunapokea na kuhifadhi aina fulani za data ya binafsi kila unapowasiliana nasi mtandaoni. Kwa mfano, tunatumia vidakuzi na teknolojia za ufuatiliaji (kufahamu zaidi, tazama Ilani yetu ya Vidakuzi) wakati kivinjari chako kinapofikia tovuti au matngazo yetu na maudhui mengine yanayotolewa na au kw aniaba ya Upfield kwenye tovuti nyingine.
Mifano ya aina za data za binafsi tunazokusanya ni pamoja na: anwani ya IP, kitambulisho cha kifaa, data ya eneo, tarifa ya kompyuta na muunganisho kama vile aina ya kivinjari na toleo, mipangilio ya saa za eneo, aina na matoleo ya programu jalizi ya kivinjari, mfumo wa uendeshaji na historia ya ununuzi – ambayo Upfield wakati mwingine hujumuisha na taarifa kama hiyo kutoka kwa wateja wengine. Wakati wa baadhi ya shughuli zako za kuvinjari intaneti kwenye tovuti za Upfield pia tunaweza kutumia zana za programu kupima na kukusanya taarifa ya kipindi, ikiwemo nyakati za ukurasa kufanya kazi, hitilafu za upakuaji, urefu wa ziara kwenye kurasa fulani, taarifa za matumizi ya ukurasa na mbinu zilizotumika kuvinjari mbali na ukurasa. Pia tunaweza kukusanya taarifa ya ufundi ili kutusaidia kutambua kifaa chako kwa madhumuni ya kuzuia ulaghai na uchunguzi.
Data ya binafsi tunayokusanya kutoka kwenye vyanzo vingine.
Tunaweza kukusanya data ya binafsi kutoka kwenye vyanzo vingine ikiwemo:
Kama sehemu ya shughuli zetu za kuajiri, tunaweza kukusanya taarifa binafsi kutoka kwenye tovuti za mitandao ya jamii kama vile LinkedIn (mfano, unapotumia kurasa wa Upfield / maudhui kwenye au kutuma ombi la jukumu kupitia LinkedIn).
Kategoria fulani za data ya binafsi kama vile mbari, kabila, dini, afya, jinsia au data ya bayometri huainishwa kama “kategoria maalum za data” na manufaa kutoka kwenye ulinzi wa ziada chini ya sheria ya ulinzi wa data ya Umoja wa Ulaya.
Tunaweka vikwazo pale ambapo tunakusanya na kuchakata kategoria maalum za data. Hata hivyo, tunaweza kukusanya data kama hizo katika hali zifuatazo:
Upfield inakusanya na kutumia tu data hii ya binafsi ambapo umetupa kibali chako dhahiri ili tufanye hivyo au pale tunapohitajika kisheria kuchakata data kama hizo. Katika hali nyingine, huenda ukatupa taarifa ambayo haihusishi moja kwa moja ukusanyaji wa kategoria zozote maalum za data, lakini inayoweza kumaanisha au kupendekeza dini, afya yako au kategoria nyingine maalum za data.
Tunakusanya, kuchakata na kufichua data yako ya binafsi kwa madhumuni yafuatayo:
Tunapokusanya na kutumia data yako ya binafsi kwa madhumuni mengine yoyote, tutakufahamisha kabla au wakati wa ukusanyaji.
Pia tunaunda wasifu kwa kuchanganua taarifa kuhusu kuvinjari kwako mtandaoni, tabia ya kutafuta na kununua na matumizi yako ya mawasiliano ya chapa yetu kwa kuunda sehemu (kuunda vikundi ambavyo vina sifa fulani zinazohusiana) na kwa kuweka data yako ya binafsi kwenye sehemu moja au zaidi. Kwa maelezo zaidi kuhusu hii, tazama "Profiling", hapa chini.
Tunategemea maslahi halali kwa ujumla kwa ajili ya kuchakata data yako ya binafsi (mradi tu maslahi yetu halali yasipuuzwe na maslahi yako ya ulinzi wa data au haki na uhuru msingi). Maslahi yetu halali yanaweza kuwepo kwa mfano ukijisajili ili upokee taarifa kuhusu moja ya chapa zetu au uingie kwenye shindano na tutumie data ya binafsi tuliyokusanya ili kuelewa vyema mahitaji ya wateja wetu.
Katika hali nyingine, tunachakata data yako ya binafsi ili kuunda kandarasi ambayo wewe ni au utakuwa mhusika. Kwa mfano, tunahitaji kuchakata data yako ya binafsi ili tukuruhusu kushiriki kwenye moja ya mashindano yetu, au kukutumia sampuli ambazo umeomba.
Pia tunachakata data yako ya binafsi tukiwa na jukumu la kisheria (mfano, majukumu ya ushuru au usalama wa jamii) kufanya mchakato kama huo. Kwa mfano, agizo la mahakama au hati ya kuitwa mahakamani inaweza kutuhitaji kuchakata data ya binafsi kwa madhumuni maalum.
Inapofaa (kama vile ikiwa tunakusanya data ya binafsi ya kategoria maalum kwa madhumuni yanayohusiana na mzio, tafiti za hiari kuhusu bidhaa zetu (mfano, athari zao kwenye viwango vya kolesteroli) au sababu tofauti za wafanyakazi), tutaomba kibali chako cha kuchakata data ya binafsi. Pale ambapo umetoa kibali cha kuchakata shughuli, una haki ya kuondoa kibali chako wakati wowote. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kufanya hivi, tafadhali tazama sehemu ya Wasiliana Nasi hapa chini.
Kama mashirika mengi yanayopatikana kwenye mtandao, Upfield hutumia data yako ya binafsi kuunda wasifu. Tunaunda wasifu kwa kuchanganua taarifa kuhusu kuvinjari kwako mtandaoni, tabia ya kutafuta na kununua na matumizi yako ya mawasiliano ya chapa yetu kwa kuunda sehemu (kuunda vikundi ambavyo vina sifa fulani zinazohusiana) na kwa kuweka data yako ya binafsi kwenye sehemu moja au zaidi. Sehemu hizi hutumiwa na Upfield kuboresha tovuti na mawasiliano yetu kwako (kama vile kuonyesha maudhui yanayofaa kwako iunapotembelea tovuti yetu au katika jarida kwako) na kuonyesha ofa na matangazo yanayofaa kutoka chapa za Upfield kwenye tovuti za Upfield na kupitia tovuti nyingine. Sehemu zinaweza pia kutumiwa kwa kampeni nyingine kwenye tovuti za Upfield. Upfield huunda data yako kwa kutumia vidakuzi ambapo umetupa vibali vya kufanya hivyo; kwa mfano, kukubali mipangilio ya vidakuzi kwenye kivinjari chako mtandaoni. Kwa maelezo zaidi, tazama Ilani yetu ya Vidakuzi [kiungo].
Ikiwa umeomba kupokea barua au mawasiliano ya SMS kutoka kwetu, tunafuatilia ikiwa umefungua, kusoma au kubofya maudhui ili kuona unachovutiwa nacho ili tukupe maudhui tunayodhani unaweza kufurahia.
Tunatumia data hii kuunda unavyopendezwa na kutopendezwa navyo. Kwa mfano, tukiona kuwa unatazama resipe za Vegan mara kwa mara kwenye tovuti yetu na ulichagua kupokea barua pepe kutoka kwetu, tunaweza kukupa taarifa kuhusu resipe mpya za Vegan ambazo zimeingia kwenye tovuti kwa maslahi yako, au tunaweza kuboresha maudhui ya wavuti wetu unapotembela vitu tunavyodhani utavutiwa navyo.
Kulingana na taarifa hii ya wasifu, pia tunaweza kukupa matangazo tunayodhani kuwa utayapenda na unataka kuona unapotazama maudhui kutoka kwetu au kutoka kwenye mtandao wetu wa wachapishaji tunaotangaza nao. Wakati mwingine tunaweza kutumia mahali ulipo kukupa matangazo yanayohusiana na promosheni au matukio yanayotendeka karibu nawe tunayodhani kuwa unaweza kuvutiwa nayo.
Pia tunaweza kutumia taarifa uliyotoa kwa wahusika maalum na kukubali kushirikiwa, kama vile umri, jinsia, hatua ya maisha na mambo mengi yanayokuvutia ili kutambua watu tunaodhani watakuvutia pia na tunaoamini watavutiwa na matangazo kama hayo.
Katika hali nyingine, Upfield huchakata data yako ya binafsi kwa kutumia njia ya kiotomatiki. Uamuzi wa kitomatiki ni uamuzi ambao unatolewa kwa njia ya kiotomatiki pekee ambapo hakuna binadamu wanaohusika kwenye mchakato wa kufanya uamuzi unaouhusiana na data yako ya binafsi. Kwa mfano:
Hatutafnaya maamuzi kulingana na uamuzi unaofanywa kiotomatiki pekee ulio na athari kubwa kwako. Tukifanya hivyo tunakuarifu na kukupa taarifa wazi kuhusu uamuzi wetu kutegemea mchakato wa kiotomatiki ili kufanya uamuzi wetu na msingi wetu we kisheria kwa kufanya hivyo. Kwa mfano, Upfield huchakata data yako ya binafsi kwa kutumia njia ya kiotomatiki ikiwa ni muhimu tu kwa ajili ya kuweka ndani au utendakazi wa kandarasi nawe, au wakati umetoa kibali chako dhahiri.
Una haki ya kutokuwa mhusika wa uamuzi unaotokana na mchakato wa kiotomatiki na unaotoa athari za kisheria au athari nyingine kubwa kwako. Una haki ya:
Kama biashara ya kimataifa, Upfield hushiriki data yako ya binafsi kindani na wahusika waliochaguliwa katika hali zifuatazo:
Data yako ya binafsi itahamishwa na kuchakatwa katika nchi ambazo si nchi ambayo wewe ni mkazi. Nchi hizi zinaweza kuwa na sheria za ulinzi wa data ambazo ni tofauti na sheria za nchi yako.
Hata hivyo, tumechukua kinga zinazofaa ili kuhitaji data yako ya binafsi kuendelea kulindwa kwa mujibu wa Ilani hii ya Faragha. Kwa mfano, kinga zetu zinajumuisha kutekeleza European Commission’s Standard Contractual Clauses za uhamisho wa data ya binafsi hadi wahusika wengine wasio wa EEA na kati ya kampuni zetu, unaohitaji kampuni zote kulinda data ya binafsi zinazochakata kutoka EEA kwa mujibu wa shweria ya ulinzi wa darta ya Umoja wa Ulaya. Taarifa zaidi kuhusu kinga hizi zinapatikana unapoomba.
Upfield inatilia maanani sana usalama wa data yako ya binafsi. Tunatumia kila jitihada kulinda data yako ya binafsi dhidi ya matumizi mabaya, uharibifu, kupotea, ufikiaji usioidhinishwa, marekebisho au ufichuaji.
Hatua zetu zinajumuisha kutekeleza udhibiti wa ufikiaji unaofaa, kuwekeza katika uwezo wa kisasa wa usalama wa taarifa wa kulinda mazingira ya IT tunayookoa na kuhakikisha kuwa tunasimba kwa njia fiche, kutumia jina bandia au kutotambulisha data ya binafsi pale inapowezekana.
Ufikiaji wa data ya binafsi unaruhusiwa tu miongoni mwa waajiriwa na mawakala wetu kwa msingi wa haja ya kujua na kulingana na majukumu ya usiri wa mkataba wakati unachakatwa na wahusika wengine.
Tunaweka data yako ya binafsi tunayokusanya pale tunapokuwa na hitaji la biashara halali kufanya hivyo na tunaiweka tu kwa muda usiozidi unavyohitajika ili kutimiza madhumuni yake ya awali ya kukusanya. Kwa mfano, unapotutumia swali mtandaoni, tutaweka data ya binafsi kwa kipindi kinachotuwezesha kushughulikia au kujibu malalamishi yoyote kuhusu jibu au swali lako.
Data yako pia inaweza kuwekwa ili tuweze kuendelea kuboresha hali yako ya utumiaji nasi na kuhakikisha kuwa unapokea zawadi zozote za uaminifu unazostahiki.
Tunaweza data ya binafsi tunayokusanya moja kwa moja kwa madhumuni kwa muda mfupi iwezekanavyo, ambapo baadaye tunaweka hatua za kuifuta kabisa.
Tutaipitia data ya binafsi tuliyo nayo na kuifuta kwa usalama, au kuitoa utambulisho wakati mwingine wakati si hitaji tena la kisheria, biashara au mteja kuwekwa. Ikiwa hili haliwezekani (kwa mfano, kwa sababu data yako ya binafsi imehifadhiwa kwenye kumbukumbu ya ziada), kisha tutahifadhi data yako ya binafsi kwa usalama na kuitenga kwa uchakataji wowote zaidi hadi ufutaji uwezekane.
Unaweza kudai haki hizi wakati wowote. Tumetoa muhtasari wa haki hizi hapa chini pamoja na kile ambacho hii inakuhusu. Unaweza kudai haki zako kwa kutuma barua pepe au kwa kuwasilisha ombi kupitia fomu ya “Wasiliana Nasi” kwenye tovuti zetu.
Una haki zifuatazo za ulinzi wa data:
Ikiwa una maswali au masuala yoyote kuhusu matumizi yetu ya data yako ya binafsi, tafadhali wasiliana nasi ukitumia maelezo yafuatayo: Upfield.Privacy@upfield.com
Tutasasisha Ilani hii ya Faragha inapohitajika ili kuakisi majibu ya wateja na mabadiliko katika bidhaa zetu. Tunapochapisha mabadiliko kwenye Ilani hii ya Faragha, tutarekebisha tarehe “iliposasishwa mwisho”. Ikiwa mabadiliko ni makubwa, tutatoa ilani kuu zaidi (ikiwemo arifa ya barua pepe ya mabadiliko ya Ilani ya Faragha).
Mbali na Ilani hii ya Faragha, huenda kukawa na kampeni au promosheni mahususi ambazo zitaongozwa na masharti au ilani za ziada. Tunakuhimiza usome haya kabla ya kushiriki katika kampeni au promosheni zozote kama hizo.